Mbeto amtaka OMO aachane na stori za Uchaguzi uliomalizika

 ……….

Ma Mwandishi  Wetu  Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  kimemtaka aliyekuwa Mgombea Urais  wa Zanzibar  kupitia ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman  , iwapo  chama chake kina ubavu wa kushindana na CCM kisubiri Uchaguzi Mkuu ujao  mwaka 2030.

Aidha ,CCM  kimeyaita madai ya kutaka Uchaguzi Mkuu  wa Zanzibar  urudiwe huku OMO   akiamini  atamshinda Rais Dk Hussein  Ali Mwimyi amesema hizo ni mbwembwe na maneno ya  faraja kwa wafuasi wake.

Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanziabr  Idara  ya Itikadi  Uenezi na Mafunzo Khamis  Mbeto  Khamis amesema hayo huku akimtaka OMO aachane na  stori za Uchaguzi kwakuwa ukurasa huo umeshafungwa rasmi.

Mbeto  alisema inashangaza  kukisikia ACT kikidai  kuwa kilishinda wakati wananchi wameshampigia kura Rais Dk Mwinyi  ambaye  sasa , anaiongoza Serikali  na kujipanga kuleta maendeleo yatakayoonekana.

“Mwambieni OMO aache porojo badala yake aende  ikulu akaape kuwa Makamo wa Kwanza  wa Rais. Ikiwa ameshindwa kazi awapishe wenzake washirikiane na Rais Dk Mwinyi  kuiletea maendeleo  Zanzibar ” Alisema Mbeto 

Katibu huyo Mwenezi aliongeza kusema ACT  kiache kuidanganya dunia badala yake kikubali ukweli  nguvu  za ushindi wa CCM  zimetokana na haiba  ya ustawi wa Maendeleo  yanayoonekana hivi  sasa Unguja na Pemba. 

‘Ile zama ya  kusambaza propaganda  uchwara kupitia  radio vifua na watu kuwadanganyana vibarazani  imepita. Wananchi hawataki kushabikii  siasa za chuki na migawanyiko ‘Alieleza 

Mbeto alisema  madai kuwa uchaguzi ukirudiwa tena Rais Dk Mwimyi hatapata  kura asilimia 30,mbeto ameyaita hayo  ni maneno yasioingia akili na kuaminika. 

Alieleza kuwa kwa wakati  huu  hadithi  za uchaguzi mkuu hazina nafasi hata ya kusikilizwa au kufuatiliwa na wananchi,  badala yake watu wanaitarajia SMZ  izidi kuongeza kasi ya mabadiliko kiuchumi, kisiasa na kijamii.

“Uchaguzi wa Mwaka  1995 wapo wakiodai  Dk Salmim  Amour ataondoshwa  kabla ya Mwaka 200.Wakasema tena  Dk Amani Karume hamalizi muda wake. Walipokataa kushirikiana na Dk Ali Mohamed  Shein SUK iliundwa na kusongambele “Alisema Mwenezi  huyo.