Masalanga: Tulizidiwa, ila bado tuna nafasi

BAADA ya Singida Black Stars kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya CR Belouizdad katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, kipa wa timu hiyo, Hussein Masalanga amezungumzia wapinzani wao walikuwa wazuri kutokea pembeni.

Masalanga amesema bado wana matumaini makubwa ya kushinda mechi zijazo ili kutinga robo fainali ya CAF, lakini hakusita kukiri kufanyia kazi udhaifu waliouonyesha.

“Mechi ilikuwa ngumu eneo ambalo wapinzani wetu walikuwa hatari ni kushambulia kutokea pembeni, naamini kocha kayaona mengi ambayo atatuelekeza,” amesema Masalanga na kuongeza;

MASA 01


“Wachezaji tunahamasishana ili kuendelea kukaa katika morali ya mechi, kila mmoja wetu anatamani kuona tunashinda nyumbani, mcheza kwao hutunzwa, tunajua itakuwa ngumu lakini tunajipanga.”

MASA 02


Amesema anatamani kuona timu nne za Tanzania zinatinga hatua inayofuata ili kuandika historia ya aina yake katika michuano hiyo baada ya sasa kuandika historia mpya kwa kuingiza timu zote nne makundi.