SIMBA imepoteza mechi ya kwanza ya kimataifa nyumbani tangu ilipolala 3-0 mbele ya Raja Casablanca Februari 18, 2023, lakini lawama zote za mechi ya leo zilienda kwa kocha wa Wekundu hao ambaye alianza kushambuliwa na mashabiki tangu kilipoanikwa kikosi kilichovaana na Petro Atletico ya Angopla.
Simba ilicharazwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, huku kikosi hichio kikianza pambano bila ya straika baada ya nyota watatu wanaocheza nafasi hiyo, Jonathan Sowah, Seleman Mwalimu ‘Gomes’ na Steven Mukwala wakianzia benchi.
Kitendo cha washambuliaji hao kuanzishwa benchi kulifanya mashabiki kupitia ukurasa wa akaunti ya Instagram kulilaumu benchi la ufundi na wengi wanaamini ndio iliyowaponza kupoteza kwa mara ya kwanza mechi ya awali ya makundi tangu 2018.
Mashabiki wa Simba walionyesha wasiwasi juu ya kikosi kilichoanza na baadhi kuamua kutoa maoni yao katika akaunti hiyo ya Simba kuponda uamuzi wa benchi hilo la ufundio lililopo chini ya Dimitar Pantev na Seleman Matola.
Shabiki anayetambulika kwa Paul Clement92: aliandika; Kocha unazingua mbona hamna streika’
Mwingine Minja-phoneland aliandika; Mbona kocha muoga huyu tunaanzaje bila namba 9 leo?
Huku shabiki mwingine zombie.son akatoa povu lake kwa kuandika; Safu ya ufungaji vp wakuu 😢 mbn wote nje
Mwingine aliohoji iweje kocha anamuamini Neo Maema kuliko mastraika wake, japo wengine walitetea uamuzi huo wa kuanzishwa benchi kwa mastraika hao watatu wa kikiosi hicho.
Hata hivyo, kile kilichowatoa povu mashabiki wa Simba kilionekana uwanjani kwa timu hiyo kushindwa kuwapa raha Wanasimba kwa Joshua Mutale alietumika kama mshambuliaji wa katikuzidiwa ujanja na mabeki wa wageni.
Hii ni mechi ya nne mfululizo kwa Simba kushindwa kupata ushindi nyumbani katika michuano ya CAF kwani awali ililazimishwa sare tatu kuanzia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita dhidi ya RS Berkane na mechi mbili za raundi ya awali kwa msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini.
Bao la kiungo Jonathan Toro dakika ya 78 kwa shuti la nje ya eneo la hatari lilitosha kuamua mchezo huo likimgonga beki wa a Simba na kumpoteza kipa Yakub Seleman na kujaa wavuni.
Kocha wa Simba, Dimitar Pantev katika kikosi cha leo atalazimika kujilaumu kwa kuanza na kikosi ambacho hakikuwa na mshambuliaji halisi akimuanzisha kiungoJoshua Mutale kama mshambuliaji wa kati, huku akiwaweka benchi washambuliaji Seleman Mwalimu, Steven Mukwala na Jonathan Sowah aliyemuingiza dakika ya 52.
Kipindi cha kwanza timu zote licha ya kushambuliana kwa hesabu zilishindwa kufunga kwa kiwango kikubwa zikicheza kwa tahadhari kubwa.
Ndani ya dakika 45 za kwanza kila timu ilitengeneza shuti Moja lililolenga lango dakika ya 44 ikitangulia Petro kupitia kiungo wake Pedro Gagal aliyepiga shuti hafifu lakini kipa Yakoub Suleiman alidaka Imara.
Shambulizi hilo likaimsha Simba ambao nao dakika hiyo hiyo ikafanya shambulizi la haraka ikitengeneza nafasi nzuri shuti la Ellie Mpanzu likapanguliwa na kipa Hugo Marques
Nafasi kubwa ambayo Simba itaijutia kipindi cha kwanza Ile iliyotengeza dakika ya 22 krosi ya Shomari Kapombe ilimkuta Joshua Mutale ambaye alitengeneza nafasi nzuri kwa Morris Abraham lakini shuti lake likagonga mwamba na kurudi mchezoni.
Pedro alitengeneza nafasi nyingine akiwachambua mabeki wa Simba, lakini shuti lake likatoka nje kidogo na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na kasi Mpanzu tena alitengenezewa nafasi nzuri na Morice kisha kumtoka kipa lakini shuti lake likatoka nje kidogo dakika ya 51.
Baada ya kumalizana na Petro, Simba itarudi mazoezi kabla ya kusafiri wiki hii kuifuata Stade Malien ya Mali katika mechi ya pili ya kundi hilo itakayopigwa wikiendi hii mjini Bamako ikihitaji kupata ushindi ili kujiweka pazuri katika Kundi D lenye mabingwa wa zamani wa Afrioka, Esperance ya Tunisia waliolazimishwa suluhu nyumbani na Stade Malien juzi usiku..
Mara baada ya mechi hiyo ya pili ya kimataifa, Simba itarudi katika Ligi Kuu Bara.
Simba imepangwa kukutana na TRA United katika mechi itakayopigwa Desemba 3 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabiora kisha kufunga hesabu za mwaka 2025 dhidi ya Azam Desemba 6. Mechi zote zikiwa ni viporo.
SIMBA: Yakoub, Kapombe, Mligo, Nangu, Rushine, Kante, Mutale, Naby, Maema, Morice na Mpanzu
PETRO: Hugo, Anderson, Ruben, Toro, Bernardo, Pereira, Kinito, Eddie, Mabululu, Hossi na Pedro