Tanzania kujiuliza kwa New Zealand Futsal

BAADA ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Futsal kupoteza mechi ya kwanza ya kundi C ya michuano ya Kombe la Dunia la Futsal kwa mabao 10-0 dhidi ya Ureno, leo saa 7 usiku itakuwa na kibarua kingine cha kutafuta pointi tatu.

Mashindano hayo yanayoendelea nchini Ufilipino ikiwa hatua ya makundi na Tanzania iliyopo kundi C ilianza vibaya kwa kupokea kichapo hicho kikubwa kutoka kwa Ureno.

Hata hivyo, sio Tanznaia pekee iliyopokea dozi ya maana lakini mechi ya kundi D, Panama iliyotandikwa mabao 17-0 na Italia, New Zealand ilitandikwa mabao 6-0 dhidi ya Japan, Morocco iliyopo kundi A ilianza vibaya kwa kufungwa mabao 6-0 dhidi ya Argentina sawa na Ufilipino iliyopoteza mbele ya Poland.

TANZ 01

Hivyo Tanzania ni miongoni mwa timu zilizopokea vipigo vizito lakini timu iliyoweka rekodi zaidi ni Panama ya kuruhusu mabao 17.

Tanzania sasa ina mechi nyingine ya kujiuliza hatma yake kwenye michuano hiyo mikubwa Duniani mbele ya New Zealand ambayo nayo ilipoteza mechi iliyopita.
    
Mechi hiyo itapigwa Uwanja wa PhilSports Arena, Pasig saa 7 usiku kwa saa za Ufilipino lakini kwa Tanzania itakuwa kesho saa 2 kamili asubuhi.

TANZ 02

Tanzania leo inahitaji ushindi au angalau sare ili kuwarudisha mchezoni wachezaji baada ya kupoteza mechi iliyopita ambayo wengi kujiamini kulipungua kuliposababisha kufanya makosa yaliyoigharimu timu hiyo.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Curtis Reid alisema wanafahamu ugumu wa mechi hiyo lakini amewaandaa wachezaji kiakili kuikabili New Zealand.

CAF 01

“Tulikuwa na kazi kubwa ya kuwaweka sawa wachezaji na wabaki kwenye mchezo hiyo tumeifanya kwa asilimia kubwa, tumeangalia ubora na udhaifu wa New Zealand mechi iliyopita na tumejipanga kuhakikisha madhaifu yao tuyatumie,” amesema  Reid.