Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) amewafutia kesi na kuwaachia huru washtakiwa 47 waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kutenda kosa la uhaini.
Wakili wa Serikali Mkuu, Job Mrema, akishirikiana na Cathbert Mbiling’i, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ya uchunguzi wa awali (PI) namba 26645 ya mwaka 2025 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Mrema ametoa taarifa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo, kuwa DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo kwa washtakiwa 47 kati ya 48 waliopo katika kesi hiyo.
Hata hivyo, washtakiwa hao wamefutiwa kesi chini ya kifungu namba 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.

Mheshimiwa hakimu akiwa mahakamani alisema kuwa Jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi hii isipokuwa mshtakiwa Nasrim, washtakiwa mnajulishwa kuwa kifungu hiki kilichotumika kuwafutia kesi ndicho kinachoweza kutumika kuwakamata tena iwapo Jamhuri itajiridhisha kuona ushahidi upo, watawarudisha wanaweza kurudishwa mahakamani
Related
