WAKATI Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwaachilia huru washtakiwa 20, kati ya 22 wa kesi ya uhaini inayotokana na maandamano ya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Mfanyabiashara Jennifer Jovin maarufu kama Niffer (26) amerudishwa rumande.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo leo Jumanne Novemba 25, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati inayoitwa Nolle Prosequi ( taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendela na mashtaka dhidi ya washtakiwa) kwa mujibu wa kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai marejeo ya mwaka 2023″.
Mbali na Niffer, mshtakiwa mwingine ambaye DPP anayo nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yake ni Mika Chavala (32)
