MIKOPO YA MILIONI 290 YATOLEWA KWA MAKUNDI MAALUMU CHATO

…………………..

CHATO 

HALMASHAURI ya wilayani Chato mkoani Geita imetoa mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 294 kwa vikundi vya wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu ili kuinua uchumi wa makundi hayo.

Fedha hizo ni utekelezaji wa agizo la serikali kwa kila halmashauri za wilaya, Manispaa na Majiji nchini kutenga kiasi cha aslimia 10 ya mapato yake ya ndani kwaajili ya kuyakopesha makundi hayo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 294,000,000 kwa vikundi 32 kati ya vikundi 62 vilivyokidhi vigezo vilivyowekwa na serikali, Katibu tawala wa wilaya ya Chato Thomas Dimme, kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo, Louis Peter Bura, amesema pesa hizo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan, kutoa mikopo hiyo ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa kuwa rais wa Tanzania mwaka 2025.

Vile vile amesema mikopo hiyo inakusudiwa kuwanufaisha walengwa ili kujikwamua ki uchumi na kwamba siyo pesa za kwenda kufanya anasa.

Kauli ya mkuu huyo wa wilaya inaungwa mkono na methali ya Kifaransa inayosema ” Yeye anayengoja kuvaa viatu vya marehemu anaweza kutembea peku muda mrefu” kumbe kusubiri maendeleo yatokee pasipo kufanya kazi kwa bidii ni kama unaishi kwa kungoja viatu vya marehemu.

Aidha baadhi ya vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo ni pamoja na vikundi vya wanawake 20, vijana 13 na wenye ulemavu vikundi 6 katika jimbo la Chato Kaskazini na Chato kusini.

Bura amesisitiza kuwa pesa hizo ni mikopo isiyokuwa na riba na kwamba inatazamiwa kuonyesha matokeo chanya kwa jamii na kwamba waliokopeshwa wanapaswa kurejesha mikopo yao kwa wakati ili kutoa fursa kwa walengwa wengine kunufaika na mpango huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Mandia Kihiyo, Ofisa maendeleo ya jamii wilayani humo, Elimkwasi John, amempongeza Rais Samia, kwa kuridhia halmashauri za wilaya nchini kutoa mikopo ya aslimia 10 kwa makundi maalumu.

Kadhalika amesema hatua hiyo ni miongoni mwa mikakati ya halmashauri hiyo kukusanya fedha zaidi ya shilingi bilioni 2.8 katika bajeti ya mwaka 2025/26 ili kuongeza upatikanaji wa mikopo ya aslimia 10 kwa vikundi vyenye sifa.

Mpango huo wa serikali kwa makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu unapaswa kupongezwa kwa kuwa umelenga kusaidia jamii kuinua kipato na kujiondolea umaskini, kama ilivyo kauli ya Mwanamuziki maarufu na mwanzilishi wa miondoko ya Raggae duniani, Robert Nesta Marley raia wa Jamaica aliyewahi kusema “rafiki wa kweli ni kama nyota, utamtambua wakati wa giza litakapokuwa limekuzunguka” 

Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo, Stephania William kutoka kikundi cha wanawake Iparamasa pamoja na Samwel Kisumo, wamesema wanakusudia kujiondolea umaskini wa vipato kutokana na mikopo hiyo ambayo wamepata kutoka serikalini na kwamba watakuwa tayali kurejesha kwa wakati ili kutoa mwanya kwa wengine kunufaika na mikopo hiyo.

                         Mwisho.