NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Wito huo umetolewa leo Novemba 27, 2025 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Waandishi yanayofanyika kila Novemba chuoni hapo.
Prof. Palangyo amesema kuwa lengo kuu la siku hiyo ni kutoa hamasa kwa vijana, watoto na watu wazima kuunda maandiko bunifu sambamba na kuinua hali ya usomaji wa vitabu katika jamii.
“Kila mtu ana wazo, kila mtu ana kitu cha kuandikwa; kile kinaposomwa na wengine kinazaa mambo mengine mengi. Tunataka hali ya kupenda kusoma iwe asili yetu,” alisema Prof. Palangyo.
Ameongeza kuwa matumizi ya akili ya asili yana nafasi kubwa na ya kipekee isiyofananishwa na kitu kingine, hususani katika uandishi bunifu.
Kwa upande wake, Prof. Fredrick Mtenzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, amesema kuwa AI itumike kama chombo cha msaada katika uandishi, si kuchukua nafasi ya mawazo ya kibunifu ya mwandishi.









