Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kesi ya kudharau amri ya Mahakama iliyokuwa imefunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche yametupiliwa mbali
Akisoma uamuzi wa Mahakama hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa kwa hati ya dharura amesema, Mahakama imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima.Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahakamani hapo nje ya muda
Jaji Mbagwa amesema kesi ya msingi namba 8960/2025 iliyoko chini ya Jaji Hamidu Mwanga ndio iliyokuwa msingi wa kesi iliyokuwa mbele yake, na kwamba amri ya Mahakama kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA ilitolewa na Mahakama Juni 10.2025
Aidha, Jaji Mbagwa ameendelea kufafanua kuwa kesi ya kudharau amri ya Mahakama ililetwa Mahakamani hapo Oktoba 03 mwaka huu takribani siku 106 jambo ambalo halikubaliki kisheria, Sheria inataka maombi ya aina hiyo yaletwe ndani ya siku 60.
Related
