WANAWAKE MKOA WA DODOMA WAMLILIA DKT MAHUNDI

……………

Na Ester Maile Dodoma 

 Naibu Waziri wa maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Marryprisca Mahundi amesema kuwa wizara hiyo inatarajia Kuanzisha kliniki itakayo wawezesha wanawake wote Nchini kupatiwa mikopo kwa masharti nafuu.

Naibu Waziri Mahundi amebainisha hayo leo 28 Novemba 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na wanawake wa mkoa huo katika ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuwa naibu Waziri kwenye Wizara hiyo

Aidha Mahundi amewataka wanawake kupatiwa Mwanasheria atakaye kuwa akiwasaini barua zao kwa gharama nafuu pale watakapo hitaji kwenda kuchukua mikopo .

Hata hivyo Naibu waziri amemwagiza Naibu Katibu wa wizara hiyo Amon Mpanju kufanya mazungumzo na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) pamoja na wakala wa viwango (TBS) ili kuweza kutatua changamoto zinazo wakabili wanawake katika biashara zao hasa kwenye Kodi pamoja na kupatiwa ruhusa ya kuuza bidhaa nje ya Nchi.