Mwimbaji nyota na mkongwe wa R&B duniani, Joe Thomas, amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kutumbuiza katika viwanja vya Leaders Club, huku ujio wake ukipokelewa kwa shangwe na hamasa kubwa kutoka kwa wapenzi wa muziki na wadau wa utalii.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki kikamilifu katika tukio hilo kama sehemu ya mkakati wake wa kuhimiza na kukuza utalii wa matukio (MICE & Events Tourism).
TTB imeeleza kuwa matukio kama haya yanaongeza mwonekano wa nchi, yanakuza uchumi kupitia wageni wanaotembelea Tanzania, na yanaimarisha nafasi ya Taifa kama eneo zuri na la kipekee barani Afrika
Ujio wa Joe Thomas unaongeza hamasa katika msimu wa matukio, huku Tanzania ikiendelea kuthibitisha kaulimbiu yake Tanzania Unforgettable.