Katika mazingira yasiyotarajiwa, mahafali ya 18 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yameshuhudia kuibuka kidedea kwa wahitimu bora wanne wakiwa na GPA ya 4.7 kila mmoja.
Mahafali haya yalihudhuriwa na wanajumuiya ya DUCE,wananchi wa Temeke, wazazi, ndugu na marafiki, huku yakiheshishwa na Mgeni Rasmi, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wahitimu wenzake, Bw. Sasila Masalu alisema anashukuru Uongozi wa Chuo kwa kuwaandalia Mahafali.
Aidha, aliwashukuru wazazi, walezi na hata walimu waliotambua umuhimu wa elimu na kuwasomesha kuanzia ngazi za chini hadi ngazi za stashahada na digirii.
Pia, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kugharimia masomo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Akidai kuwa kama si mikopo hii, wengi wao wasingefikia hatua hiyo kutokanana uwezo mdogo
Hata hivyo, aliiomba Serikali iendelee kujenga mazingira wezeshi kwetu ili waweze kujiajiri katika sekta mbalimbali nchini huku akiahidi kuwa wahitimu watatoa mchango mkubwa katika kuiendeleza Tanzania katika uchumi wa viwanda.
Katika mahafali haya, Chuo kiliwatunuku wahiimu 1,823 katika ngazi ya digirii na stashahada huku wahitimu wa kike wakiwa ni 55.3% na wanaume wakiwa ni asilimia 44.7%


