Hamza kumfuata Camara Morocco kwa matibabu

WAKATI kipa namba moja wa Simba, Moussa Camara akitarajiwa kufanyiwa upasuaji kesho Jumanne Novemba 18, 2025 huko Morocco, beki wa kati Abdulrazack Mohamed Hamza naye ametajwa kuwa mbioni kwenda nchini humo kwa ajili ya matibabu ya goti. Camara ambaye huu ni msimu wake wa pili akiwa na wekundu hao wa Msimbazi, aliondoka nchini jana Jumapili…

Read More

Sowah, Mutale wampa jina jipya kocha Simba

BAADHI ya mastaa wa Simba, wakiwamo Jonathan Sowah na Joshua Mutale wamemtungia jina jipya kocha anayesimamia mazoezi ya viungo, Mohamed Mrishona ‘Xavi’ wakimuita kwa sasa ‘Mr Quickly Quickly’ kutokana na kufanya mambo yake kwa uharaka. Xavi amesema kiongozi wa utani huo ni mshambuliaji Sowah kila anapomwona anamwita kwa jina hilo, wengine ni Shomari Kapombe, Joshua…

Read More

Dakika 540 za Msuva Iraq

WINGA wa Kitanzania, Simon Msuva hajaanza vyema Ligi Kuu Iraq akiwa na kikosi cha Al Talaba SC baada ya kucheza dakika 540 na kufunga bao moja. Ni msimu wa pili kwa winga huyo wa zamani wa Wydad AC ya Morocco na Yanga, kuitumikia Talaba, ambako msimu uliopita alifunga mabao 12 kwenye mechi 11. Msimu huu…

Read More

Clara ajipanga kuvunja rekodi yake Saudia

NYOTA wa Kitanzania, Clara Luvanga amesema anapambana kuhakikisha kila msimu anavunja rekodi zake mwenyewe za misimu iliyopita. Hadi sasa, Clara anaongoza kwenye mbio za ufungaji bora ikiwa ni raundi ya sita ya Ligi Kuu ya Wanawake Saudia akiweka kambani mabao 11 na asisti tatu. Akizungumza na Nje ya Bongo, Clara amesema kwake ni faraja kuona…

Read More

Maniche afichua siri ya Mnigeria Mtibwa Sugar

KOCHA Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma ‘Maniche’, amesema beki wa timu hiyo, Mnigeria Victor Chukwuemeka Collins, ameanza taratibu katika kikosi hicho kwa sababu kuu mbili, ambapo ya kwanza ni ugeni wake na ya pili ni kutozoea Ligi. Akizungumza na Mwanaspoti, Maniche amesema beki huyo wa kati anahitaji muda zaidi wa kuzoeana na wachezaji wenzake…

Read More

Singida Black Stars yafunguka ishu ya Lyanga, Mpepo

UONGOZI wa Singida Black Stars umesema nyota wawili wa timu hiyo, Ayoub Lyanga na Eliuter Mpepo, bado wana mikataba ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho msimu huu, licha ya kudaiwa kutokuwa kwenye mipango ya timu hiyo na huenda wakaachwa. Ofisa Habari na Mawasiliano wa Singida, Hussein Massanza, aliliambia Mwanaspoti nyota hao wote wawili bado wana mikataba…

Read More

Azam FC kuifuata AS Maniema kiakili

KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka nchini keshokutwa Jumatano kwenda DR Congo kuiwahi mechi ya kwanza ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Maniema Union, huku kocha wa timu hiyo ya Chamazi, Florent Ibenge akitambia maandalizi waliyofanya. Mechi hiyo itapigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Stade des Martyrs, Kinshasa DR Congo, huku timu…

Read More