TEC yahimiza uchunguzi huru vurugu Oktoba 29, Katiba Mpya
Dar es Salaam. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limekemea vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025, huku likitoa wito wa uchunguzi huru utakaoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa kidemokrasia ufanyike. Mbali na hilo, TEC limetaka watu wote waliokamatwa kabla, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kuachiwa huru. Sambamba na hilo, baraza hilo, limekumbushia kuanza kwa mchakato…