Mawakili wa Heche Waomba Siku Tatu kuwajibu Jamhuri
Na Mwandishi Wetu MAWAKILI wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche katika shauri la kushikiliwa kwa kiongozi huyo, wameiomba Mahakama iwape siku tatu kwa ajili ya kufanya utafiti na kujipanga kujibu pingamizi za upande wa Jamhuri. Mawakili hao wakiongozwa na Selemani Matauka akisaidiana na mawakili Fredrick Msacky, Paul…