Profesa Kabudi: Tawasifu za viongozi ni dira ya taifa katika vipindi vya misukosuko

Arusha. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema endapo waasisi wa Taifa hili wangeandika tawasifu zao wenyewe ikiwemo mitikisiko na changamoto walizopitia, ingesaidia kujua mapito ambayo Taifa liliwahi kupitia na ingekuwa ni dira ya sasa hasa katika vipindi hivi vya mitikisiko na namna ya kuiendea. Profesa Kabudi ameyasema hayo jana usiku…

Read More

Dk Mwigulu ataka Watanzania kuwakataa wachonganishi

Arumeru. Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kulinda amani na kuwakataa watu wachache wanaochochea, kuwachonganisha, kuvuruga amani, na kuharibu miundombinu inayogharimu fedha za umma, ikiwemo ile iliyojengwa kwa nguvu za wananchi. Amesema vijana na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kutambua kuwa wakichagua kuifukuza amani, wamechagua kuongeza umaskini. Dk Nchemba amesema hayo alipozungumza na wananchi katika…

Read More

Wahitimu wanne wa DUCE waibuka kidedea mahafali ya 18; Waipongeza serikali kwa ufadhili

Katika mazingira yasiyotarajiwa, mahafali ya 18 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yameshuhudia kuibuka kidedea kwa wahitimu bora wanne wakiwa na GPA ya 4.7 kila mmoja.  Wahitimu hawa ni Ramadhani Raphael Seif(Bachelor of Education in Science), Gonelimali Roland Julius (Bachelor of Science with Education) na Benedicto Mwamini Scharion na Sasila Masalu (Bachelor…

Read More

Dk Mwigulu amwagiza IGP kuacha kumtafuta Askofu Gwajima

Arumeru. Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura kuondoa tamko la kumtafuta Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na badala yake wamwache ajitokeze aendelee na ibada zake ili wajenge umoja wa kitaifa. Hatua hiyo inakuja siku saba baada ya Dk Mwigulu kuagiza kufunguliwa kwa…

Read More

Meneja wa Yusuph Athuman afichua jambo

MENEJA wa Yusuph Athuman anayekipiga Napsa Stars inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia, Hon Simbeye amesema kama mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga ataendelea kupata nafasi ya kucheza huu unaweza kuwa msimu wake bora. Kabla ya kutimkia Zambia msimu uliopita alisajiliwa na Yangon United inayoshiriki Ligi Kuu Myanmar kabla ya kurejea Tanzania na kumaliza mkataba wake…

Read More

Kilio cha vijana kwa Serikali

Mbeya. Uhaba wa ajira, uhuru wa kujieleza, ukimya wa Serikali kuhusu matukio ya utekaji, na ugumu wa upatikanaji mikopo ni baadhi ya changamoto zilizozaguliwa na vijana, wakitaka ifanyie kazi kwa maslahi ya Taifa. Vijana wameishushia Serikali mzigo huo katika wiki mbili za ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka,…

Read More

RAIS SAMIA: POLISI WAACHE KUMTAFUTA DKT. GWAJIMA

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliagiza Jeshi la Polisi liache kumtafuta Askofu Dkt. Josephat Gwajima kama walivyokuwa wametangaza awali ili aweze kuendelea shughuli zake. Amesema baada ya kutoa msamaha kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, waumini wanahitaji wamuone kiongozi wao, hivyo anatakiwa ajitokeze hadharani aendelee na kazi yake. “Mwacheni…

Read More

Tume kuchunguza yaliyotokea Oktoba 29 kupingwa kortini

Dar/Arusha. Baada Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha matukio ya wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, limefunguliwa shauri mahakamani la maombi ya kibali cha kuipinga uhalali wake. Shauri hilo la madai mchanganyiko limefunguliwa Novemba 26, 2025 katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo, Dar es Salaam na mwanaharakati Rose…

Read More

Takwimu za mbwana Samatta Le Havre

INGAWA nahodha wa timu ya taifa Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta hajafunga bao lolote akiwa na kikosi cha Le Havre ya Ufaransa katika dakika 518, takwimu zinaonyesha ni mchezaji hatari anapokuwa ndani ya boksi. Samatta alijiunga na Le Havre Agosti 05 mwaka huu akitokea PAOK inayoshiriki Ligi Kuu ya Ugiriki alipoitumikia misimu miwili akiipa ubingwa…

Read More