TTB Yatakiwa Kuongeza Utafiti Kubaini Vivutio Vipya vya Utalii
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ameutaka uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuongeza juhudi katika kufanya utafiti wa kubaini vivutio vipya vya utalii, ili kuimarisha ushindani na kuongeza idadi ya watalii nchini. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisi za TTB, Dkt. Kijaji amesema…