Watanzania waitwa kupima magonjwa yasiyoambukiza bure
Dar es Salaam. Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia Ijumaa, Novemba 28 hadi Jumapili, Novemba 30, 2025, kupima magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) bure. Katika kambi hiyo kutafanyika uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo kiharusi, magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na shinikizo la juu la damu. Kutatolewa pia matibabu…