Wizara ya Madini yafuta leseni 73 za uchimbaji, utafiti
Dodoma. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amezifuta leseni 73 za uchimbaji na utafiti, akisisitiza kuwa kazi hiyo itakuwa endelevu kwani hakuna leseni inayotolewa kama mapambo. Leseni zilizofutwa zinajumuisha 44 za utafiti na 29 za wachimbaji wa kati. Leseni hizo ni miongoni mwa 205 ambazo wamiliki wake waliandikiwa hati za makosa na kutakiwa kujibu kwa kuyarekebisha…