Vikundi 82 vyanufaika mkopo wa Sh789 milioni Chunya
Mbeya. Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imetoa mkopo wa zaidi ya Sh789.5 milioni kwa vikundi 82 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Mikopo hiyo imetolewa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali linaloelekeza halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya kuwezesha makundi hayo kiuchumi….