BoT kuja na kanuni kuwabana wakopeshaji mitandaoni
Dodoma. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa imeanza kuandaa kanuni mahususi zitakazodhibiti wakopeshaji wa mitandaoni wanaotoa huduma zao bila kufuata taratibu, ikiwemo kutosajiliwa rasmi kama inavyotakiwa kisheria. Hatua hii imekuja kufuatia malalamiko lukuki kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakitozwa riba kubwa kupita kiasi na hata kudhalilishwa hadharani kupitia simu au mitandao ya kijamii wanapochelewa…