FYATU MFYATUZI: Inakuwaje Fyatu mzima anajigeuza au kugeuzwa mdudu?
Kunguni na chawa ni mojawapo ya wadudu wachafu, na hatari bila kusahau wawafugao miongoni mwa viumbe waliolaaniwa tangu walipoumbwa. Ni dhalili, dhalimu, katili, na tegemezi. Hawana akili, aibu, maarifa, wala huruma. Ni hatari, hatarishi, na wabaya hakuna mfano. Hunyonya hata maiti na mizoga. Ni watumwa wa matumbo yao yasiyoshiba. Huishi kwa kunyonya wengine na kuwasababishia…