Wauza mkaa wa miti kukiona Songwe
Songwe. Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayotajwa kuchangia kushuka kwa uzalishaji wa zao la kahawa, Serikali mkoani Songwe imepiga marufuku mtu yeyote kujihusisha na shughuli za mkaa unaotokana na miti. Imesisitiza kuwa bila kuchukua hatua za haraka na makusudi kwa kuoneana aibu, miaka 10 ijayo dunia inaweza kuharibika na kuondoa sekta ya kilimo hicho…