VODACOM YAENDELEA KURUDISHA SHUKRANI KWA WATEJA WAKE

 Ofisa wa M-Pesa kutoka Vodacom Tanzania Plc Evelyn Mwinuka akikabidhi Kapu kwa moja ya wateja wa kampuni hiyo Lukas Njabeki Chuma, ikiwa ni  ishara ya kurudisha shukrani kwa wateja wa kampuni hiyo. 

Tukio hilo limefanyika eneo la Ipinda-Kyela jijini Mbeya ikiwa ni muendelezo wa Vodacom Tanzania na msimu wa sikukuu wakigawa makapu ya sikukuu maeneo mbalimbali nchini.

Meneja mauzo wa Vodacom Tanzania Plc mkoa wa Iringa, Zidiel Mbwambo akikabidhi Kapu la sikukuu kwa Rehema Robert Mwang’onda ikiwa ni ishara ya kusherehekea na wateja wa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu. Tukio hili limefanyika eneo la Ipinda – Kyela, jijini Mbeya