Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela Mohamed Mussa (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc Philip Besiimire na viongozi wengine wa Vodacom mara baada ya kampuni hiyo kukabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwamo vitimwendo (wheelchairs), karatasi za nukta nundu kwa ajili ya wasioona pamoja na vifaa vingine lukuki, vifaa hivyo vimetolewa katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Watu wenye ulemavu inayoadhimishwa leo (Tarehe 3 Disemba 2025).
Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mhesimiwa Waziri akiambatana na Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Wazazi na Wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na viongozi waandamizi wa Vodacom Tanzania waliokuwa Mjini Unguja mwanzoni mwa wiki hii.