Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Geita limemchangua diwani wa kata ya Lutede iliyopo mamlaka ya mji mdogo wa Katoro ndugu Jumanne Misungwi kuwa mwenyekiti wa baraza hilo.
Ni katika kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita ambapo jumla ya madiwani 51 katika wilaya hiyo wameapishwa kuitumikia Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti Misungwi amewashukuru madiwani hao kwa kumuamini na kumchagua kuwa kiongozi wa vikao vya madiwani vitakavyokuwa vinafanyika.
Aidha amewaomba ushirikiano ili kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo katika halmashauri hiyo.

.jpeg)


