………….
Na Ester Maile Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amewataka viongozi wa dini nchini kutumia nguvu kubwa kuliombea taifa ili yasitokee matukio ya uvunjifu wa amani kama ilivyokuwa Oktoba 29, mwaka huu wakati wa uchaguzi mkuu.
Senyamule, ameyabainisha hayo leo 05 Desemba 2025 jijin Dodoma wakati akifungua kongamano la maombi ya viongozi wa dini mbalimbali lililofanyika jijini Dodoma.
Amesema wananchi pia wanajukumu la kulinda amanu ya nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Desemba 9 ambapo kumekuwepo na baadhi ya makundi ya watu kudai kufanya maandamano siku hiyo katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Vile vile amesema kuwa kutakuwa na maombi maalumu yakuiombea nchi na mkoa wa Dodoma kuanzia tarehe Disemba 7 na kilele cha maombi hayo ni Desemba 9 ili kuiweka nchi katika hali ya usalama .

