Wagosi wanazitaka pointi tatu za Yanga

BAADA ya kuambulia sare ugenini dhidi ya Mashujaa, kocha mkuu wa Coastal Union, Mohamed Muya amesema wana dakika 90 ngumu kuwakabili watetezi wa Ligi Kuu Bara katika mechi itakayopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mechi hiyo itakayopigwa kuanzia saa 1:15 usiku jijini Dodoma kutokana na kufungiwa kwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ikiwa ni kati ya mechi mbili zitakazopigwa siku hiyo ikiwamo ya Dabi ya Mzizima itakayopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Muya amesema anafahamu wanacheza na timu bora iliyo na wachezaji bora wanaendelea na maanadalizi mazuri ili waweze kuwendana na kasi ya wapinzani wao.

Muya amesema wataingia katika mechi hiyo kwa kuwaheshimu Yanga kwa sababu ndio watetezi, lakini hawana hofu kwani na wao wanaamini wapo ligi kuu kwa ajili ya kushindana dakika 90 zitaamua ubora.

COA 01

“Yanga ni timu bora Afrika na ina wachezaji wengi wazuri huu mchezo tunauchukulia kwa ukubwa wachezaji wangu pia wanatambua umuhimu wa huo mchezo malengo ni kukusanya pointi tatu;

“Hautokuwa mchezo rahisi, lakini tunaendelea na maandalizi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuonyesha ushindani kwa wapinzani wetu ambao nakiri kuwa ni bora kutokana na aina ya kikosi walichonacho.”

Muya amesema sare waliyoipata dhidi ya Mashujaa ugenini imekuwa ya thamani kwao na imewaweka katika nafasi nzuri kwani malengo kwa asilimia kubwa yametimia sasa wanajiandaa kutumia vyema Uwanja wa nyumbani wa Jamhuri Dodoma wakiikaribisha Yanga.

NAB 01

“Ligi ni ngumu hakuna mechi rahisi Yanga ni bora na sisi pia ni bora malengo yetu na wao ni tofauti kwenye kuwania taji tu lakini kucheza ligi kila msimu sisi pia tunatamani kuwa hivyo kuhusu kutwaa taji kwa msimu huu hatuna malengo hayo zaidi tunataka nafasi tano za juu,”

“Tunaendelea na maandalizi na matarajio ni  kukutana na timu nzuri iliyo na wachezaji wengi bora ambao ukiondo ligi wanashiriki michuano mikubwa ya Ligi ya Mabingwa hawawezi kuwa rahisi bila mipango imara.”