DRC. Mapigano yametokea tena Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuanzia jana Ijumaa, ikiwa siku moja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuwakutanisha viongozi wa Congo na Rwanda mjini Washington kutia saini mikataba mipya inayolenga kumaliza mgogoro.
Juzi Alhamisi Desemba 5, 2025, Rais wa Congo Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda walithibitisha ahadi zao kwa makubaliano yaliyofikiwa Juni mwaka huu ili kuleta utulivu katika nchi hiyo na kufungua njia kwa uwekezaji zaidi wa madini wa Magharibi.
“Tunasuluhisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa miongo kadhaa,” alisema Trump, ambaye amewaita viongozi hao ili kuhakikisha wanafikia makubaliano.
Hata hivyo, mapigano makali yameendelea huku pande zinazopigana zikilaumiana.
Kundi la waasi la AFC/M23 linaloungwa mkono na Rwanda, liliteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Congo mapema mwaka huu.
Vikosi vinavyoiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeendeleza mashambulizi yao katika maeneo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, huku vikitumia ndege za kivita, ndege zisizo na rubani na mizinga,” ameandika kwenye mtandao wa X.
Msemaji wa Jeshi la Congo amethibitishia Reuters kwamba mapigano yametokea Ijumaa katika eneo la Kaziba, Katogota na Rurambo katika Kimbo la Kivu Kusini.
“Kuna wakazi wanaokimbia makazi yao Luvungi kutokana na mabomu ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda. Wanabomoa bila kujali,” amesema.
Wawakilishi wa Jeshi na Serikali ya Rwanda hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Ofisa mwandamizi wa AFC/M23 ambaye hatutaka kutajwa jina lake, ameieleza Reuters kwamba waasi wamerejesha udhibiti wa mji wa Luberika na wameidungua ndege isiyo na rubani ya Jeshi la Congo.
“Vita vinaendelea ardhini na havina uhusiano wowote na kutiwa saini kwa makubaliano yaliyofanyika jana huko Washington,” amesema.
