Ibenge achekelea rekodi mpya kwa Simba

SIMBA bado wanalaumiana kufuatia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Azam FC, huku wenzao wanacheka tu na kumfanya kocha Florent Ibenge achekeleeΒ  kubadilisha mzimu wa matokeo mabaya dhidi ya Wekundu hao.

Iko hivi. Ibenge hajawahi kuifunga Simba ikiwa Tanzania tangu aanze ukocha katika mechi za mashindano walizokutana.

Rekodi zinaonyesha, Ibenge amewahi kukutana na Simba mara sita kabla ya hivi karibuni kutua Azam na ndani ya mechi hizo, alishinda mbili pekee tenaΒ  yeye (Ibenge) akiwa nyumbani alipokuwa anaifundisha AS Vita (5-0) na RS Berkane (2-0), huku mechi moja pekee alipoteza nyumbani (1-0) dhidi ya Wekundu hao walipokuwa na Vita zote zikiwa michuano ya CAF.

IBE 01

Ibenge hakuwahi kushinda katika mechi tatu alizocheza akiwa nchini dhidi ya Simba, kwani alipigwa (2-1) kisha (4-1) alipokuja na AS VitaΒ  pia kupoteza (1-0) alipokuja na RS Berkane kwa mechi ya marudiano.

Hivyo ushindi wa wikiendi iliyopita, Ibenge akiiongoza Azam kushinda 2-0 dhidi ya Simba unakuwa wa kwanza kwa kocha huyo kuupata dhidi ya wekundu hao.

Kama haitoshi hiyo inakuwa clean sheet ya kwanza kupata mbele ya Simba akikutana nao hapa nchiniΒ  akini kiujumla inakuwa ya tatu katika mechi zote alizokutana na Wekundu wa Msimbazi hao.

Akizungumzia hatua hiyoΒ  Ibenge alisema amefurahishwa na kubadilisha matokeo hayo mabaya ya hapa nchini dhidi ya Simba, akisema yalikuwa yanamtesa kwa muda mrefu.

IBE 02

Ibenge aliwapongeza wachezaji kwa kuipigania timu hiyo ambapo licha ya ugumu wa mchezo huo walivaa ujasiri na kutafuta ushindi muhimu kwao.

β€œNi kweli ni mara yangu ya kwanza kushinda hapa ninapokutana na Simba. Zipo mechi huko nyuma nilikuwa nakaribia kupata ushindi, lakini mwishoni mambo yakabadilika,” alisema kocha huyo raia wa DR Congo aliyeajiriwa kutoka Al Hilal ya Sudan.

β€œKatika mechi iliyopita kwanza niwapongeze wachezaji wangu niliwaambia kama tunaweza kuwa jasiri tunaweza kuandika historia nzuri na wakafanya hivyo.”

Hadi sasa Azam ni kati yaΒ  timu zilizocheza mechi chache za ligi ikiwa na tano tu kama Simba na Singida Black Stars ikivuna pointi tisa, ikishinda mbili na sare tatu.

Pia Azam ni kati ya timu mbili ambazo hazijapoteza hadi sasa katika Ligi ikiwamo Yanga iliyocheza mechi sita na kuvuna pointi 16Β  ikishinda tano na kutoka sare moja.