MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wageni wote wanaowasili mkoani humo kwa ajili ya sikukuu za Christmas na Mwaka mpya kuhakikisha wanailinda amani ambayo wameikuta.
Babu ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa, kwa sasa wameanza kupokea wananchi wengi wanaofanya shughuli nje ya mkoa ambapo kwa sasa wamerejea kwa wazazi wao.
“Wengine wamerejea nyumbani kwa ajili ya kufanya mila za kufagia makaburi huku wengine wamekuja kusalimia ndugu jamaa na marafiki” Alisema Babu.
Alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wageni wote kwani walitoka Kilimanjaro kwenda mikoa mingine kutafuta ambapo pia ujio wao utachangia kuongeza mapato ndani ya mkoa.