TANZANIA YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA SEOUL SMART CITY PRIZE 2025

Na Mwandishi Weru Seoul, Korea Kusini

Internet Society Tanzania Chapter (ISOC-TZ) imetunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Seoul Smart City Prize 2025, kutambua mchango wake mkubwa katika kuboresha huduma za afya kupitia teknolojia ya kidijitali, hususan kupitia Mradi wa SmartJiji Public Health, unaotekelezwa chini ya Tanzania Digital Inclusion Project (TADIP).

TADIP ni sehemu ya Mradi mkubwa wa Kitaifa unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ujulikanao kama Digital Tanzania Project, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Mradi huu unalenga kuongeza ujumuishi wa kidijitali, huduma bunifu za kijamii na matumizi ya teknolojia kwa maendeleo ya wananchi.

Tuzo hii ya hadhi ya kimataifa ilikabidhiwa na Mheshimiwa Oh Se-hoon, Meya wa Jiji la Seoul, ambaye alisifu mchango wa ISOC Tanzania Chapter katika kuleta suluhisho bunifu za teknolojia kwa ajili ya kuboresha maswala ya afya kwa wananchi kwa ubunifu wa kidigiti.

Hafla hiyo muhimu ilishuhudiwa pia na Mheshimiwa Balozi Togolani Mavura, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, aliyewapongeza wadau wote wa ISOC-TZ na Serikali kwa ushirikiano unaozaa matunda katika maendeleo ya kidijitali.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Dr. Nazarius Nicholas Kirama (PhD), Rais wa shirika la Internet Society Tanzania Chapter, alisema tuzo hiyo ni ushahidi wa kazi kubwa inayofanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali, wadau wa maendeleo na asasi za kiraia katika kuhakikisha huduma za kidijiti zinawafikia wananchi wote.

Kupitia TADIP, kama sehemu ya Digital Tanzania Project inayotekelezwa na Serekali ya Tanzania kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, tunaona kwa vitendo jinsi teknolojia inavyobadilisha maisha ya watu. Tunaingia mwaka 2026 tukiwa na hamasa mpya, maarifa mapya na dhamira kubwa ya kuleta mageuzi makubwa zaidi.

Tuzo ya Seoul Smart City Prize hutolewa kwa taasisi zinazochangia kwa katika kujenga miji janja (smart cities) kwa kutumia teknolojia, ubunifu na ushiritwaji wa wananchi