Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jopo la Serikali Mbalimbali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) Sir Jim Skea kuhusu uwezeshwaji wa nchi uwezo wa kuandaa na uoembuzi wa taarifa za kisayansi kuhusu hali ya mazingira. Majadiliano hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-7 unaoendelea jijini Nairobi, Kenya Desemba 11, 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akishiriki Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA-7) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya Desemba 11, 2025 ambapo aliwasilisha mafanikio ya Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa ya Mazingira (MEAs) wakati wa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa.
.jpg)
