BURIANI JENISTA MHAGAMA – MICHUZI BLOG

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Mongella, wakitoa heshima za mwisho kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Mhe. Jenista Joakim Mhagama, mara baada ya ibada, leo Jumamosi, tarehe 13 Desemba 2025.  

Shughuli ya utoaji wa heshima za mwisho kuaga mwili wa Mhe. Jenista Mhagama iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska, Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma, iliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.