SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), limemchagua Rais wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu Afrika (ACA), Eng. Hersi Said kuwa miongoni mwa wataalam watakaofundisha kwenye kongamano kubwa la mpira wa miguu litakalofanyika Doha, Qatar, kesho Jumapili, Desemba 14, 2025.
Katika kongamano hilo, Hersi amepangiwa na FIFA kufundisha kwenye mada ya Mfumo wa Mabadiliko ya Klabu.
Miongoni mwa Wataalam wengine wa mpira wa miguu duniani watakaozungumza kwenye kongamano hilo ni kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, Roberto Di Mateo (kocha wa zamani wa Chelsea), Dennis Wise (kiungo wa zamani wa England na Chelsea), Alexander Pato (kiungo wa zamani wa Brazil na AC Milan) na Eric Abidal (beki wa zamani wa Ufaransa na Barcelona).
Hersi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Klabu za Soka za Wanaume Duniani, ndiye mtaalamu pekee wa mpira wa miguu kutoka Afrika aliyepata nafasi ya kufundisha kwenye kongamano hilo.