WINGA Mtanzania, Kassim Mbarouk aliyeitumikia Sauti Parasports amejiunga na Dispas SC ya Uturuki kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mbarouk anakuwa mchezaji wa nne kutoka Tanzania kujiunga na Ligi ya Walemavu nchini Uturuki baada ya Ramadhan Chomelo, Shedrack Hebron (Sisli Yeditepe) na Mudrick Mohamed wa Mersin.
Akizungumza na Mwanaspoti Mbarouk amesema alipata dili hilo akiwa na chama lake la zamani Sauti Parasports walioshiriki mashindano yaliyoandaliwa na Azam, miezi michache iliyopita na alipokuwa na timu ya Burundi.
Aliongeza kuwa baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya CECAFA nchini Burundi wachezaji Wakenya walimuunganisha na mabosi wa timu hiyo ndipo akakubali kusaini mkataba.
“Wachezaji Wakenya nilipokutana nao kwenye mashindano ya CECAFA niliwasumbua sana waliponiona wakawatumia mabosi wa timu details zangu ndipo nikakubaliwa kujiunga na timu hiyo,” amesema na kuongeza
“Malengo ni kwenda kuipambania heshima ya nchi yangu na nifanye makubwa ili tuweze kusaidia na wengine, pia hapa nina kama siku tatu nne hivi lakini kuna Watanzania wenzangu wanacheza hapa.”