DKT. MWAMBA ATEMBELEA JENGO JIPYA LA OFISI ZA WIZARA YA FEDHA.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akisikiliza taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Msimamizi wa Mradi, Bw. Hija Mrutu, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akiongozwa na Msimamizi wa Mradi Bw. Hija Mrutu, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akisajiliwa kwa kutumia mfumo wa vitambulisho wa kielektoniki na Afisa Tehama Wizara ya Fedha, Bw. Omary Waziri, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma.

………………….

Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ametembelea Jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma, ambapo amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo la kisasa linalotarajiwa kuwa ‘State of the Art’.

Dkt. Mwamba aliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda na Msimamizi wa Mradi Bw. Hija Mrutu na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha, kutembelea Ofisi mbalimbali ndani ya Jengo hilo na kujionea kazi kubwa iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo hilo ambalo linatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.

Dkt. Mwamba alipongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo hilo na kueleza kuwa zoezi la ukamilishaji wa uwekaji wa Samani litakapo kamilika watumishi wote watahamia kwenye Jengo hilo na kwamba hivi sasa baadhi ya Idara zimehamia katika Jengo Hilo.

Alisema Ofisi alizotembelea zina utulivu wa kutosha kuweza kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika mazingira bora na rafiki.

MWISHO