Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 15,2025 amewasili mjini Songea mkoani Ruvuma,ambako atashiriki Ibada ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenista Mhagama aliyekuwa Mbunge wa Peramiho na Waziri Mstaafu, inayofanyika katika Kanisa Katoliki Peramiho.
Jenista Mhagama alifariki Desemba 11, 2025 kwa maradhi ya moyo.







