MAKAMU WA RAIS DKT NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA ‘SADC ORGAN TROIKA’ KWA NJIA YA MTANDAO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ Troika) uliofanyika kwa njia ya mtandao akiwa Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 15 Desemba 2025.

Mkutano huo umejadiili hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kurejesha amani na usalama katika Jamhuri ya Madagascar.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe.