Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema kuna haja ya kubadili Mfumo wa Magereza nchini ili kuendana na kasi ya dunia huku akigusia dhamira ya serikali kupitia baadhi ya sheria ambazo tumerithi kutoka kwa wakoloni na kuzifanyia mabadiliko ili kuweza kuboresha masuala ya utoaji haki katika vyombo mbalimbali vya haki jinai ikiwemo Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza.
Ametoa kauli hiyo leo, jijini Dodoma baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji ambayo kazi yake ni Kumshauri Rais juu ya Utekelezaji wa majukumu aliyokabidhiwa Rais na ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sambamba na ujazaji wa nafasi hizo katika Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza, kama Rais atakavyotaka.
‘Ni lazima kweli tutoke kwenye magereza ya kikoloni na sasa tuje kwenye magereza ya Jamhuri ambayo ni watu huru wanaoishi katika nchi ya kidemokrasia inayotambua haki za binadamu lakini pia kuna haja ya kufanya mabadiliko ya sheria maana dunia ya sasa na kwa Uchumi tuliofikia lazima tufanye mabadiliko ziko sheria zetu nyingine bado ni za kikoloni kwahiyo ipo haja ya kuzibadilisha na hilo litashirikisha wadau wote waliopo kwenye mnyororo huu wa sheria na masuala ya haki jinai.’ alisema Waziri Simbachawene
Akizungumza Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma,Mheshimiwa, Dkt. Juliana Masabo amepongeza mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kwenye vyombo vya usalama vilvyopo chini ya wizara akikiri mabadiliko hayo yanasaidia mchakato wa utolewaji haki na kupunguza badhi ya mambo ikiwemo masuala ya upelelzi kuchelewa.
‘Nakiri kuna mabadiliko sana hasa magereza niliyotembelea masuala ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano yamesaidia kesi kuendeshwa kwa haraka kwa kesi kwa njia ya mtandao jambo ambalo linasaidia ufanisi wa utendaji wa sekta ya mahakama lakini pia kuna masuala ya haki za binadamu kuna mabadiliko makubwa sana katika magereza yetu hali inayopelekea utu wa mtuhumiwa au mahabusu kuwa ni mzuri katika magaereza yetu.’alisema Jaji Dkt.Masabo.


.jpeg)
.jpeg)
