Benki ya NMB imekabidhi vifaa tiba na mahitaji mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 15 kwa Kituo cha Afya Makole jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuimarisha huduma za afya kwa jamii.
Msaada huo unalenga kusaidia kituo hicho kuboresha utoaji wa huduma za afya na kukidhi mahitaji ya wananchi wanaopata huduma katika eneo la Makole na maeneo jirani.
Vifaa hivyo vilipokelewa na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole, Dkt. Revocatus Kitena. Uwakilishi wa Benki katika hafla hiyo uliongozwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango, akiambatana na baadhi ya Mameneja wa Matawi wa NMB Kanda ya Kati.
.jpeg)

.jpeg)
