TUZO YA JAFO YA UFANISI WA JUU KWA MRADI WA MAENDELEO KUANZA KUTOLEWA KILA MWAKA KWA MWENYEKITI WA KIJIJI

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Na.Alex Sonna-,Kisarawe

MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ametangaza kuanza kutolewa kwa Tuzo ya Jafo ya Ufanisi wa Juu kwa Mradi wa Maendeleo, ikiwa ni mpango wa kutambua na kuhamasisha utendaji bora, ubunifu na uwajibikaji miongoni mwa Wenyeviti wa Vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

Akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wilayani humo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dkt. Jafo amesema tuzo hiyo (JAFO’s High Perfomance Development Project Award), inalenga kukuza ufanisi wa juu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, kuongeza uwajibikaji na kuibua ushindani chanya miongoni mwa wenyeviti hao.

Amesema tuzo hiyo itatolewa kila mwaka ili kumtambua na kumzawadia Mwenyekiti au Mwakilishi wa Kijiji aliyeonesha utendaji wa hali ya juu, ubunifu na matokeo yanayopimika katika kusimamia mradi ndani ya Halmashauri hiyo

“Tuzo hii ni kwa Mwenyekiti wa Kijiji au mwakilishi wa kijiji atakayeng’ara kwa mafanikio ya kipekee katika kuibua, kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi, hususan ile yenye athari chanya katika sekta za afya, elimu, kilimo, biashara, michezo na miundombinu, ninalenga kuhamasisha viongozi wetu wa vijiji kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uwazi zaidi. Tunataka kuona matokeo halisi yanayogusa maisha ya wananchi,” amesema Dkt. Jafo.

Mbunge huyo ameongeza kuwa tathmini ya mshindi wa tuzo hiyo itazingatia vigezo mbalimbali, ikiwemo utekelezaji wa miradi yenye athari kubwa ndani ya muda uliopangwa, maboresho yanayopimika katika utoaji wa huduma, usimamizi bora wa rasilimali, ushiriki wa wananchi na wadau pamoja na uendelevu wa miradi iliyotekelezwa.

Amesema pia tuzo hiyo itahusishwa moja kwa moja na mradi au mpango mahsusi wa maendeleo, ambapo ushahidi wa matokeo kama ongezeko la ufanisi, ubora wa huduma na kuridhika kwa wananchi utatumika kama msingi wa tathmini.

Awali, Dkt. Jafo amepongeza mchango mkubwa wa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, akisema wao ni kiungo muhimu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali ngazi ya msingi.

Ameeleza kuwa mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wake wa uongozi wa miaka 2025–2030, akisisitiza dhamira ya kufanya kazi kwa kasi ya ‘chaka kwa chaka’ ili kuharakisha maendeleo vijijini.

Amebainisha kuwa kupitia usimamizi bora wa viongozi wa vijiji, azma ya kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati ifikapo mwaka 2030, pamoja na kuimarisha sekta ya elimu na shughuli za kiuchumi, itawezekana kwa vitendo.

“Ndani ya miaka mitano ijayo tunahitaji kufanya kazi kwa mchakamchaka, kuanzia ukusanyaji wa mapato hadi matumizi yake, ili miradi ya maendeleo isimamiwe kwa ufanisi na kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi,” amesisitiza.

Nao baadhi ya wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamempongeza Dkt Jafo kwa ubunifu huo, wakisema kuwa utaongeza hamasa na ushindani chanya wa kimaendeleo katika Halmashauri ya Kisarawe.

Wamesema tayari wamejipanga kikamilifu kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili kuongeza ufanisi na hatimaye kuibuka washindi wa tuzo hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,aakiwasili katika ukumbi wa halmashauri wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuzungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri hiyo ya ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Nyahori Mahumbwe,wakati ,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Aidan Kitare,,wakati ,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Afisa Utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Bi.Sabra Mwankenja wakati ,akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.