Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso leo Disemba 16, 2025 akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa kubwa la kisasa la maji la Kidunda ambalo kwa sasa ujenzi wake umefikia 40%
Ujenzi wa Bwawa hilo ni maamuzi magumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha changamoto za maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani inakuwa historia.
Aidha kwa kutambua umuhimu wa maji Serikali kupitia wizara ya maji imekuwa na mikakati na mipango endelevu ya kuwa na miradi ya kisasa ya maji ambayo italeta suluhisho la kudumu la kukosekana kwa maji safi na salama katika nyakati zote hususani kiangazi hivyo ujenzi wa Bwawa la Kidunda Mkoani Morogoro ni moja ya mkakati kabambe wa kukabiliana na changamoto ya kukosekana kwa maji.
Mwisho Bwawa hilo la Kidunda linatarajiwa kukamilika mapema mwakani 2026 licha ya kutoa huduma ya maji Bwawa hilo linatarajiwa kuzalisha umeme takribani megawatt 20 kwa saa ambazo zitaenda kuongezwa katika gridi ya taifa.


.jpeg)



