BENKI YA CRDB YASHIRIKIANA NA KIDS’ HOLIDAY FESTIVAL KUKUZA ELIMU YA FEDHA KWA WATOTO

 Sambamba na udhamini huo, Benki ya CRDB itatoa ufadhili wa masomo kwa washindi wanne watakaopatikana katika matamasha mawili yatakayofanyika tarehe 20 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam na tarehe 27 Desemba 2025 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kids’ Holiday Festival, Geraldine Mashele. Kupitia ushirikiano huu, Benki ya CRDB inalenga kuunganisha burudani na elimu kwa vijana kwa kutoa elimu ya fedha, uwekezaji na akiba kwa kundi la vijana ambalo ni msingi wa maendeleo ya taifa letu.