DKT. MWIGULU: AMANI NI MSINGI WA MAENDELEO

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 18, 2025 amezungumza na wakazi wa Kiwira mkoani Mbeya ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya umma na mali za watu binafsi ambazo zimeathirika na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaeleza wananchi hao kuwa kila Mtanzania anapaswa kuilinda amani iliyopo kwani ndio msingi wa maendeleo. “Kila mtanzania anapaswa kuilinda Tanzania”

Amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuwa makini na watu wenye nia ovu dhidi ya Tanzania na kuhamasisha vurugu zinazoathiri shughuli za kiuchumi na kijamii.

“Tunaelewa lengo lao ni rasilimali zetu, Tanzania ina rasilimali adhimu barani Afrika na wanajua ili kuzipata ni lazima kuwavuruga watanzania ambao wameungana, hili msikubali amani yetu ndio kila kitu”.