KIKAO KAZI CHA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS NA MAAFISA HABARI WA SERIKALI LEO

Mshauri wa Rais Masuala ya Habari na Mawasiliano Ndugu Tido Mhando akizungumza katika Kikao Kazi cha Kitaifa cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Maafisa Habari wa Serikali katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Desemba, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Gerson Msigwa akizungumza kwenye Kikao cha Maafisa Habari na Maafisa Mawasiliano kutoka Wizara, Halmashauri pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Desemba, 2025
 Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akiwa kwenye majadiliano kuhusu ukusanyaji maoni na mwelekeo wa Kurugenzi ya Mawasiliano katika Kikao Kazi cha Kitaifa cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Maafisa Habari wa Serikali kilichofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Desemba, 2025.
Mhariri Mtendaji wa Maudhui Mtandaoni na Ubunifu kutoka Mwananchi Communications Ltd, Zourha Malisa akielezea mada ya Usimamizi wa Mawasiliano ya Kidigitali na mitandao ya kijamii katika Kikao Kazi cha Kitaifa cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Maafisa Habari wa Serikali kilichofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Desemba, 2025.
Maafisa Habari na Maafisa Mawasiliano kutoka Wizara, Halmashauri pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali wakiwa kwenye siku ya pili ya Kikao baina yao na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Desemba, 2025.