WANAFUNZI CHUO WA USTAWI WA JAMII WAPEWA MBINU KUTUMIA SOKO LA AKILI MNEMBA


::::::::

Na Mwandishi Wetu 

CHUO cha Ustawi wa Jamii (ISW) leo kimewajengea uelewa wanafunzi na wahitimu wake katika kuhakikisha wanatumia Akili Unde (AI) ipasavyo, ili msaidizi muhimu katika kuweza kuchaka na kurahisisha kazi zao.

Akizungumza leo wakati wa Kongamano la 12 lililozungumzia Matumizi ya Akili Unde kwenye uwanda wa taaluma ya ustawi wa jamii,Mkuu wa Chuo cha Ustawi waJamii,

Dk. Joyce Nyoni amesema ni muhimu wasome wakatumia AI kama msaidizi na sio kwa hofu ya kupokonywa kazi.

“Tumekutana kuona ni kwa namna gani tunaweza kitumia Akili Unde hasa katika taalumu kujifunza na ujifunzaji wa wanafunzi.


Ameongeza ” Tumeona fursa ambazo zipo katika matumizi ya Akili Unde ikumbukwe kuwa wakati tunaanza kama nchi kulikuwa na hofu kwamba kazi zitapungua,fursa zitapungua na badala yake akili mnemba ndio itachukua nafasi za ajira kwa wahitimu wetu, lakini leo tumejifunza kuwa haiwezi kuchukua nafasi lakini ni fursa kwa wahitimu wetu kuitumia katika kazi.

Aidha, amewasihi wanafunzi na wahitimu kutumia Akili Unde kwa kufuata weledi wakitambua kwamba bado wanahitaji kuchaka na kufikiria na kuendelea kupata maarifa na sio tu kuhamisha wanachokipata kule ila iwasaidie katika kuchakata taarifa zao.

“Na bado kuna kile kipengele cha akili ya mwanadamu katika kufikiri na kuchakata taarifa anazopata kitu inahitaji umakini,”amesisitiza. 

Naye,Mkufunzi katika Kongamano hilo, Dk. Hellen Maziku amesema matumizi ya Akili Unde yapo kila sehemu na ndio inatumika zaidi duniani hata hivyo bado binadamu anakazi ya kufikiri kwa AI haifikiri kama yeye.

“Sasa tunakazi ya kufikiri kwasababu akili unde haiwezi kufikiri AI haiwezi kuchukua kazi za ustawi wa jamii kazi hizi zinahusisha kwenye kwa jamii na zinahusisha hisia zaidi ila AI itabadilisha namna ambayo unafanya kazi kwani utatumia kwa mambo fulani.Ni lazima tubadilishe akili zetu kwani haiepukiki,”amesisitiza Dk Maziku.








OOOOO