Kunywa kahawa uongeze miaka ya ujana wako

Unywaji wa hadi vikombe vinne vya kahawa kwa siku, huenda ukasaidia kupunguza kasi ya uzee wa kibayolojia kwa watu wanaoishi na maradhi ya akili, utafiti mpya umeonyesha.

Matokeo ya utafiti yaliyochapishwa katika jarida la BMJ Mental Health yanaonyesha kuwa unywaji wa vikombe 3–4 kwa siku unahusishwa na urefu wa Telomere yaani viashiria vya seli za uzee sawa na ta-kribani “miaka mitano ya ziada ya ujana kibayolojia” ikilinganishwa na watu wasiokunywa kahawa.

Hata hivyo, cha kuvutia ni kwamba utafiti haukupata faida yoyote ya kinga kwa watu wanaokunywa zaidi ya vikombe 3–4 kwa siku, jambo linalowiana na mapendekezo ya mashirika makuu ya afya, ya-kiwamo NHS (Mfumo wa huduma za afya wa umma wa Uingereza na FDA (wakala wa Serikali ya Ma-rekani unaosimamia na kudhibiti usalama wa vyakula, dawa, chanjo, vipodozi, vifaa tiba na bidhaa za kibaolojia).

Utafiti huo unaeleza Telomere hupungua kadiri mtu anavyozeeka. Mchakato huu ni wa kasi zaidi kwa watu walio na matatizo ya akili.

Kwa kuwa urefu wa telomere unaweza kuathiriwa na maisha ya mtu, watafiti walichunguza kama unywaji wa kawaida wa kahawa, unaweza kupunguza kasi ya kupungua huko kwa watu wenye magonjwa makubwa ya akili.

Utafiti ulihusisha watu wazima 436 waliojiunga na mradi wa Norwegian Thematically Organised Psycho-sis kati ya 2007 na 2018, huku watu  259 wakiwa na skizofrenia (ugonjwa wa akili unaoathiri namna mtu anavyofikiri, kuhisi, kuzungumza na kutafsiri uhalisia na 177 wakiwa na matatizo ya hisia.

Washiriki waliripoti kiasi cha kahawa wanachokunywa kwa siku na kugawanywa katika makundi manne: wasiotumia kahawa, wanaokunywa vikombe 1–2, 3–4, na wanaokunywa vikombe 5 au zaidi. Watafiti pia walirekodi historia ya uvutaji sigara.

Waliokunywa vikombe vitano au zaidi kwa siku walikuwa watu wakubwa zaidi kwa umri, na watu wenye skizofrenia walikunywa kahawa zaidi kuliko walio na matatizo ya hisia.

Uvutaji sigara, unaojulikana kuathiri uchakataji wa kafeini, ulikuwa wa juu, asilimia 77 ya washiriki wali-tambuliwa kuwa wavutaji kwa wastani wa miaka tisa. Walio kunywa vikombe vitano au zaidi walikuwa na historia ndefu zaidi ya uvutaji.

Watafiti walipima urefu wa telomere kwa kutumia seli nyeupe za damu na kugundua muundo wa “umbo la J”: wale waliokunywa vikombe 3–4 walikuwa na telomere ndefu kuliko wasiokunywa kabisa, huku kundi la wanaokunywa vikombe vitano au zaidi halikuonyesha faida hiyo.

Hata hivyo, kwa kuwa utafiti huu ni wa uchunguzi, waandishi wanasema hauwezi kuthibitisha moja kwa moja kwamba kahawa hupunguza seli za uzee.

Pia walikosa data kuhusu aina ya kahawa, muda wa unywaji, kiwango cha kafeini na matumizi ya viny-waji vingine vyenye kafeini.