SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa orodha ya waamuzi 17 waliopata beji za Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) kwa mwaka 2026.
Katika orodha hiyo, kuna waamuzi wa kati sita wanaocheza mpira wa miguu ambao ni Ahmed Arajiga, Nasir Salum Siyah, Ramadhan Omary Kayoko, Hery Ally Sasii, Tatu Nuru Malogo na Amina Samwel Kyando.
Waamuzi wasaidizi upande wa mpira wa miguu ni Hamdani Said Ally, Kassim Seif Mpanga, Frank John Komba, Mohamed Salim Mkono, Rajabu Ally Ramadhan, Respicious Dismas, Glory John Tesha, Zawadi Yusuf Hashim na Mary Seleman Said.
Pia kuna waamuzi wawili wa Soka la Ufukweni ambao ni Msilombo Jackson Steven na Ally Mohamed.