Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki , Vodacom Tanzania imeendelea kutoa zawadi ya sikukuu kwa Wateja wao na ikiwa mwaka huu imefiksha miaka 25 ya kuwahudumia.
Akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi hizo, Charles Makola, Meneja wa Vodacom Kariakoo,amesema katika msimu huu wa sikukuu Kampuni hiyo imekuja kutoa mkono wa sikukuu kwa wateja wao ikiwa ni utamaduni ambao kila mwisho wa mwaka huwa inatoa zawadi mbalimbali kwa Wateja wao ambapo kwa mwaka huu imekuwa na utofauti kidogo mteja atapata Kapu la vyakula.
“Katika sikukuu mwaka huu tunashukuru wateja wetu kwamba tupo nao pamoja tunawapa Kapu lililosheheni Kitoweo,Mchele, nyama ni Kapu ambalo limesheheni sana kama mnavyofahamu mwaka huu imefikisha miaka ishirini na tano, toka tumeanza kuwahudumia wateja wetu hapa Tanzania hivyo tunawashukuru na ni zaidi ya makapu 600 ambayo yanatolewa Nchi mzima na kwa Leo tupo hapa Katika Soko la Machinga Complex tukigawa zawadi,”amesema, Makola.
Kampeni hii pia imefanyika pia Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Mbeya,etc.
Meneja wa Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania kanda ya Dar es Salaam na Pwani George Nyanda (wa Kwanza kushoto), Meneja wa eneo la Kinondoni Yusuph Mngagi (wa pili kushoto) Meneja wa Eneo la Dar es Salaam mjini kati ( wa kwanza kulia) Makola Magongo wakikabidhi kapu la sikukuu kwa Dhahabu Halisi (wa pili Kulia). katika muendelezo wa kampeni ya “Tupo Nawe Tena na Tena” inayolenga kugawa makapu kwa wateja katika msimu huu wa sikukuu. Kampeni hiyo imeendelea kugawa makapu hayo katika mikoa mbalimbali nchini, Hafla hii limefanyika kwa lengo la kusherehekea pamoja na wateja katika msimu huu wa sikukuu, sambamba na kuhitimisha maadhimisho ya miaka 25 ya Vodacom tangu kuanzishwa kwake hapa nchini, na limefanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki .
.jpeg)
